Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Lusaka, Zambia
Global Publishers March 24, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika), Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia
Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) zimekumbushwa kuwa ni jukumu lao kufanya kazi kwa pamoja ili kumaliza changamoto za kiusalama zinazozikabili Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Ukumbusho huo umetolewa na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ambaye pia ni Rais wa Zambia, Hakainde Hichelema wakati anafungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya SADC uliohitimishwa jijini Lusaka, Zambia Machi 23, 2024.
Katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na mambo mengine, ulilenga kutathimini hali ya usalama katika Kanda ya SADC. Ilielezwa kuwa hali ya usalama Mashariki mwa DRC bado hairidhishi, hivyo umetolewa wito kwa nchi wanachama na washirika wa maendeleo kuchangia rasilimali ili vikosi vya kulinda amani vilivyopo huko na vingine vitakavyopelekwa, viweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Ilibainishwa kuwa suala la kutafuta amani katika Kanda ni suala la kimkataba wa jumuiya hiyo na Itifaki ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, hivyo ni wajibu kwa mataifa hayo kuungana pamoja kukabiliana na changamoto za kiusalama.
Wachambuzi wa mambo wamesema kuwa mahudhurio mazuri ya viongozi katika ngazi ya Rais, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu katika mkutano huo yanadhihirisha kuwa nchi za SADC zimedhamiria kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto ya usalama nchini Msumbiji na DRC.
Marais walioshiriki Mkutano huo ni Hakainde Hichelema wa Zambia, Emmerson Mnangwa wa Zimbabwe: Félix Tshisekedi was DRC; Lazarus Chakwera wa Malawi; Filipe Nyusi wa Msumbiji na João Lourenço wa Angola. Nchi za Tanzania na Namibia ziliwakilishwa na Makamu wa Rais, Lesotho, Waziri Mkuu na Afrika Kusini na Botswana ziliwakilishwa na Mawaziri wa Ulinzi.
Makamu wa Rais wa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Zambia, Hakainde Hichilema kando ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika), Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia.Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera.Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Makamu wa Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Nyusi.Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Zambia.Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akitazama vikundi mbalimbali vya ngoma za asili wakati akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Mulungushi kilichopo Lusaka nchini Zambia kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC Organ Troika),Nchi za Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Nchi zinazochangia vikosi katika jeshi la utayari la SADC lililopo nchini Msumbiji (SAMIM) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC).Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali.