×

Mbunge wa Buchosa Mhe. Eric Shingo Ashiriki Mazishi ya Kada wa CCM Zagallo, Nyehunge

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Sengerema Marco Zagalo amezikwa leo Mei Mosi Nyumbani kwake Nyehunge ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Eric Shigongo ameshiriki mazishi hayo.

 

Kada huyo wa CCM aliyezaliwa mwaka 1961 enzi za uhai wake ameshiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Chama hicho kwa kushika nafasi mbalimbali za ngazi ya kata pamoja na kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza mbele ya waombolezaji walioshiriki kwenye kuaga mwili wa kada huyo, Mhe. Shigongo ametoa pole kwa msiba huo mzito ambao umewakuta ndugu, jamaa na marafiki huku akitoa rai kwa waombolezaji kumuombea marehemu ili Mungu amuepushe na adhabu za kaburini na kutenda mema wangali hai.
“Tumekuja kuwafariji wenzetu, safari hii  ni yetu sote kinachotokea tunapishana muda wa nani ameanza na nani anafuata.Dini zote zinasema kufa ni haki kwa kiumbe waliombwa na Mwenyezi Mungu.Hata hivyo ni vema tukatiana moyo kwenye matatizo.

Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakielekea eneo la kumpumzisha aliyekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Sengerema, Marco Zagallo

Leave a Comment