Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Album ya Harmonize Mlimani City, Atangaza Jambo Jipya Kwa Wasanii (Picha +Video)
Global Publishers May 26, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa album ya Harmonize Mei 25, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mara nyingi anapokwenda nje ya nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.
Rais Samia amesema hayo wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amesema “Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”
“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”
“Tunakwenda Korea na mnawajua ni Wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu, kwahiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Flavour Rajab Abdul aka Harmonize mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Mzazi wa Msanii wa Bongo Flavour Harmonize, Habiba Baisa Chivalavala wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize akitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Albamu yake ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.