×

Katibu Mkuu CCM Nchimbi Atua Kwa Kishindo Buchosa, Mbunge Shigongo Afunguka – Video

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Jimbo la Buchosa, Halmashauri ya Buchosa, Nyehunge.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Jimbo la Buchosa, Halmashauri ya Buchosa, Nyehunge, leo Agosti 14, 2024, mara baada ya kuwasili na kupokelewa Mkoa wa Mwanza, kuanza ziara ya siku 2 ya kikazi mkoani humo, akitokea Mkoa wa Geita.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa – Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC – Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo.

Malengo ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 – 2024, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM, pamoja na kuzungumza na kuwasikiliza wananchi.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo ametoa salamu za wananchi wa jimbo hilo wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye leo yupo jimboni humo na ujumbe wake kwa ziara ya kikazi.

Shigongo ameelezea zaidi kuwa Wananchi wa Jimbo hilo wanahitaji Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami ndani ya Jimbo hilo ili kuongeza shughuli za uchumi nchini.

Leave a Comment