
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe leo Agosti 23, 2024 amezungumzia maandalizi wanayoendelea kuyafanya kuelekea katika mechi yao ya marudiano dhidi ya ya Vital’O ya Burundi haujaisha, licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza baina yao.
Yanga iliibuka na ushindi huo katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, na kesho Jumamosi Agosti 24, 2024 itakuwa nyumbani katika Uwanja wa Azam Complex, kwa mchezo wa mkondo wa pili.
Kocha Gamondi amesema amekiandaa kikosi chake kwenda kupambana na amewasisitiza wachazaji kucheza kwa kujituma ili kuendeleza matokeo mazuri.
Ally Kamwe ametumia muda huo kuwajibu wachambuzi mbalimbali wa soka wanaosema kuwa mshambuliaji wa wao Clement Mzize kuuzwa nje ya nchi.
“Miezi 4 iliyopita watu hawa hawa walikuwa wanasema tuachane na Clement Mzize,watu hao hao walikuwa wanasema Mzize hakuna kitu lakini leo wanasema Mzize ni hazina ya Taifa tumruhusu aende ili kukua kisoka”
“Hakuna timu anayostahili kucheza Mzize iwe nikwa fedha au kwa mpira isipokuwa anastahili kucheza Yanga pekee naomba niwambie wanayanga na watanzania kuwa Clement Mzize bado yupo sana Yanga sc” amesema Ally Kamwe