×

Shigongo: Sheria Ya Vileo Ifanyiwe Marekebisho, Ni Wajibu Wa Wazazi Kuwalinda Watoto – Video

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema ili kuhakikisha sheria ya kuwalinda watoto inakuwa na maana, ni lazima kuhakikisha mabadiliko yake yanaenda na mabadiliko ya kiulimwengu katika nyanja mbalimbali za kijamii na teknolojia.

Amesema hayo akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Ulinzi wa Mtoto ya Mwaka 2024 na kuongeza kuwa, hivi sasa kumekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara na hivyo, sheria za kuwalinda watoto zinapaswa kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

Shigongo ameyasema hayo leo Agosti 30, 2024 Bungeni, Dodoma alipokuwa akichangia mswada wa Marekebisho ya Sheria ya mtoto.

Leave a Comment