
Unachoweza kusema ni leo ndiyo leo katika uchaguzi wa kichama na mabaraza mbalimbali ya Kanda ya Pwani Chadema, ambao unafanyika Ukumbi wa Mashingo uliopo Kibamba Kibwegere Dar es Salaam.
Mpaka muda mabaraza za la wazee (BAZECHA) limeshamaliza uchaguzi wake kwa sasa Baraza la Wanawake (BAWACHA) linaendelea kufanya uchaguzi.
Baada ya hapo watafutia Baraza la Vijana (BAVICHA) na kufuatiwa na mtifuano wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ambapo kati ya aliyewakuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye kwa sasa yuko gerezani na Gervas Lyenga.
Katika eneo la tukio Boniface anawakilishwa na timu yake huko Gervas naye hivyohivyo huku umati uliofurika ukionesha shauku ya kutaka kumjua atakayeibuka kidedea kwenye nafasi hiyo.
HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/ GLOBAL PUBLISHERS
