
Mapinduzi Makubwa ya kielimu Kanda ya Ziwa Yaja: Ikiwa Maonyesho ya 7 ya teknolojia ya madini yakiendelea mkoani Geita taasisi na makamapuni mbalimbali yameshiriki katika maonyesho hayo ikiwemo makampuni yanayosambaza bidhaa mbalimbali migodini, wauzaji wa magari, mitambo nk lakini mwaka huu kitu cha kipikee ni ushiriki wa shule binafsi katika maonyesho hayo ambayo Shule za Waja na Savannah Plain ni kutoka Kanda ya Ziwa zimeshiriki maonyesho hayo pamoja na Shule za FEZA.

Miongoni mwa huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye banda na shule za FEZA ni pamoja na usahili wa wanafunzi kwa kidato cha kwanza kwa muhula mpya wa masomo wa 2025.
Akizungumza katika maonyesho hayo wakati wanafunzi walipotembelewa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari kwa lengo la kujifunza kutoka shule hiyo, Afisa Mratibu na msaili wa wanafunzi wa FEZA, Huzaifa Sizya alisema kama kawaida yao wao wamejikita kutoa elimu bora yenye viwango vya kimataifa kwa shule zenye mtaala wa Kimataifa (Feza International) na viwango vya kitaifa chini ya NECT.
Msajili huyo alisisitiza kwa kusema kuwa FEZA imekuwa ikiongoza katika matokeo ya kidato cha IV na VI kwa miaka karibu yote ikijivunia rekodi ya kutoa daraja la kwanza kwa wanafuzi wote miaka zaidi ya kumi sasa.
Ameendelea kusema kuwa FEZA sasa iko mbioni kufungua shule kanda ya ziwa ili kuwaletea jirani wananchi huduma bora ya elimu na kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza wananchi kupata huduma bora na hivyo wanafunzi wa kanda hiyo nao kupata huduma bora.
Msajili huyo alimalizia kwa kusema kuwa FEZA ina mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi ambao wanauwezo wa kimasomo darasani lakini kutokana na changamoto za familia zao hawana uwezo wa kusomeshwa hivyo pia FEZA wanafadhili wanafunzi hao hasa wale wenye uwezo mkubwa katika masomo ya Sayansi ili kutengeneza Madaktari na mainjinia wa baadae.