×

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde Alivyomkabidhi Pikipiki Mkulima wa Gairo

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde akimkabidhi zawadi ya pikipiki mkulima wa Gairo mkoani Morogoro, Said Dole baada ya kuibuka mshindi kwenye kampeni ya Vuna na Tigo Pesa, kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani na Mashariki (Tanga na Morogoro) Abdul Ally kwenye uzinduzi wa Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 Gairo mkoani Morogoro.

Katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo imewazawadia zawadi mbalimbali wateja wake ikiwemo pikipiki, baiskeli na simu janja baada ya kuibuka washindi kwenye Kampeni ya Vuna na Tigo pesa baada ya kutumia huduma za Tigo Pesa na ushirika kuuza mazao yao.

Washindi hao wamekabidhiwa zawadi hizo na Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde pamoja na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Mashariki yaani mikoa ya Tanga na Morogoro wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo uliofanyika wilayani Gairo mkoani Morogoro.

Wakiongea mara baada ya kukabidhiwa zawadi hizo washindi hao wamewataka wakulima wengine kuendelea kutumia huduma za Tigo Pesa kufanya malipo kwani wao kupata kwa zawadi hizo ni kutokana na juhudi zao katika kutumia mtandao huo na sio janja janja kama wengine wanavyodhani.

Leave a Comment