
Jumatano, Oktoba 9, 2024 – Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, ALAF Limited, kampuni inayoongoza katika kutoa suluhisho za ujenzi, kwa fahari inatangaza ufunguzi wa showroom mpya katika mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe.
Hii ni hatua inayothibitisha dhamira ya ALAF ya kutoa huduma bora na kukidhi mahitaji ya wateja hususani Mji wa Tunduma na maeneo ya jirani.
Showroom ya Tunduma inafunguliwa wakati ambapo mji unakua kwa kasi, ukichochewa na miradi mingi ya maendeleo na uwepo wake katika eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia. Kituo hiki kipya kitakuwa rasilimali muhimu kwa wakaazi na wafanyabiashara, kuwapa fursa ya kupata suluhisho za ujenzi zenye ubora wa hali ya juu kutoka ALAF bila usumbufu wa kusafiri umbali mrefu.

Akizungumuza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, aliipongeza ALAF kwa hatua hii muhimu, akisisitiza kwamba inaonyesha kujitolea kwa kampuni katika kuridhisha wateja. “Ufunguzi wa showroom hii wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja unaonyesha dhamira ya ALAF katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa Tunduma. Mpango huu utawasaidia kuokoa muda na kuwawezesha kupata suluhisho bora za ujenzi kwa urahisi,”.
Alitoa wito Kwa wakazi wa Tunduma na wafanyabiashara kutumia fursa ya showroom hii kupata ufumbuzi sahihi wa mahitaji ya bidhaa za ujenzi na thamani ya fedha kwani ALAF inajulikana kwa utoaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

Aidha alisema kwamba wakazi wa Tunduma hawana sababu ya kujenga nyumba na majengo yasiyo bora wakati ALAF iko karibu nao na inatoa bidhaa bora.
“Kama serikali, tutaendelea kuwasaidia wawekezaji wote wa Tunduma, ikiwa ni pamoja na ALAF, kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ili waweze kupata faida kutokana na uwekezaji,” alisisitiza.
Msimamizi Mkuu wa Matawi ya ALAF, Naeem Abdul, alionyesha furaha yake kuhusu ufunguzi wa showroom, akisisitiza jukumu lake katika kuimarisha uhusiano na wateja. “Tuna furaha kubwa kuzindua showroom yetu wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambayo ni uthibitisho wa mkazo wetu katika kutoa huduma bora. Nafasi hii mpya itatuwezesha kuelewa mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho kwa wakati,” alisema.
Kwa mujibu wa msimamizi huyo, ALAF imeitikia wito wa muda mrefu kuwekeza Tunduma ili kukidhi mahitaji ya wateja.
“Sisi ni kampuni inayoongoza kwa kutoa suluhishi bora za ujenzi nchini Tanzania. Tunataka kuwahakikishia wakazi wa Tunduma kwamba tuna bidhaa na huduma bora zitakazowapa thamani halisi ya fedha zao,” alisema.
Uzinduzi huo wa showroom ulihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali ndani ya Mkoa wa Songwe, ambao walipata fursa ya kuona bidhaa za ALAF na kuonana na uongozi na wafanyakazi wa ALAF.
ALAF Limited ni kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa utoaji suluhishi za ujenzi. Ilianzishwa mwaka wa 1960, na imeendelea kuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini. Kampuni ya ALAF si tu hutengeneza mabati, lakini pia huzalisha bidhaa mbalimbali zinazotumika katika shughuli za kuezeka nyumba za makazi na biashara.