Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeendelea kutoa elimu ya Ulinzi na namna ya kuimarisha Usalama wakati wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serkali za mitaa mwaka 2024 ambapo washiriki kutoka Jeshi la Magereza, Zimamoto, Idara ya Uhamiaji, na Jeshi la akiba wamepata fursa ya elimu hiyo huku wakitakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi.
Awali Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mjini Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi akawaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa lengo la mkusanyiko huo ni kutoa elimu kwa washiriki juu ya namna ya kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi hususani kwa vyombo vya ulinzi ambavyo vina dhamana ya kuwalinda watu wote ambao watashiriki zoezi la kupiga kura.
SSP Matagi ameongeza kuwa zipo sheria na kanuni ambazo zitatolewa na wawezeshaji kutoka vyombo hivyo ambapo aliwaka askari hao kuzingatia mafunzo ambayo yatatolewa huku akiweka wazi kuwa elimu hiyo imrlrnga kuwaongezea maarifa katika kutekeleza majukum yao kikamilifu bila kuvunja sheria.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Adam Tamuti akawata washiriki kufuata sheria za uchaguzi na kanuni zake ili kuepusha migongano na wananchi ama wagombea wa nafasi mbalimbali nyaki za uchaguzi wa mwaka huu na chaguzi zijazo ambapo alisema vyombo hivyo vina dhamana ya kuvisimamia.
ASP Adam akaweka wazi kuwa kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana na kuwepo kwa sheria mpya mbili zinazosimamia masuala ya uchaguzi, Sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 na sheria ya Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024 huku akisisitiza kuwa uelewa juu ya sheria hizo utasidia kusimamia sheria na kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa sheria.
Nae Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Sotery Sotery akawasisitiza askari hao juu ya namna ya kujitambulisha kwa viongozi wengine eneo ya usimamizi wa kituo cha kupiga kura ili kutambuana huku akisisitiza utimamu wa akili na mwili kuwa ni jambi la msingi la askari atakaye simamia uchaguzi.
Kwa upande wake mshauri wa Jeshi la akiba Wilaya ya Arusha akawataka askari kutambua umuhimu wa elimu hiyo ambayo itawasaidia kutekeleza majukum yao kwa usahihi wakati wote wa uchaguzi wa mwaka huu na chaguzi zijazo.