×

Makamu wa Rais Kuondoka leo kuelekea Baku Azerbaijan, Kumwakilisha Rais Samia

Makamu wa Rais,  Dkt. Philip Mpango

Makamu wa Rais,  Dkt. Philip Mpango anaondoka nchini leo Novemba 08, 2024 kuelekea Baku nchini Azerbaijan, kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 29 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 29) unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 11 Hadi 22, 2024Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaondoka nchini leo Novemba 08, 2024 kuelekea Baku nchini Azerbaijan, kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 29 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 29) unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 11 Hadi 22, 2024

Akiwa nchini Azerbaijan Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia mkutano huo ambapo ataeleza msimamo na jitihada zinazochukuliwa Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Makamu wa Rais atashiriki mikutano ya pembezoni ikiwa ni pamoja na mkutano utakaojadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, fursa za nishati safi ya kupikia na biashara ya kaboni.

Mbali na ushiriki katika mkutano wa COP 29, Makamu wa Rais anatarajiwa kufanya mikutano ya uwili na Wakuu wa nchi na Serikali pamoja na viongozi wa mashirika ya Kimataifa wanaoshiriki mkutano huo.

OLE SENDEKA KUMPIGIA MAGOTI RAIS SAMIA SIYO RC SENDIGA wa MANYARA – AJIAPIZA BUNGENI….

Leave a Comment