
Kampuni ya Meridianbet imeendelea kuwa mfano wa kampuni zinazojali jamii baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa watoto wa kituo cha UMRA Children Center kilichopo Magomeni, Dar es Salaam.
Katika msaada huo, watoto hao wamepatiwa mahitaji muhimu ya chakula yakiwemo mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku ambazo zitasaidia kuboresha ustawi wao.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram alisema kuwa kampuni hiyo imejipanga kuendelea kuwa karibu na jamii kupitia shughuli zake za CSR zinazolenga kusaidia watu wenye uhitaji na kuleta mabadiliko chanya kwa Watanzania.
“Tunajivunia kutumia nafasi yetu kugusa maisha ya watoto hawa. Tunaamini kila mtoto anastahili furaha, matumaini na mazingira mazuri ya kuishi,” alisema mwakilishi huyo wakati wa kukabidhi msaada huo.
Kwa upande wao, viongozi wa UMRA Children Center walitoa shukrani zao kwa Meridianbet wakisema msaada huo umefika kwa wakati sahihi na utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili watoto hao kila siku.