×

Afisa Tarafa wa Nyaishozi Akawakabidhi Reflectors Maafisa Usafirishaji Akihamasisha Kupiga Kura

Afisa Tarafa Ndg. Kelvin Berege akimkabidhi kiakisi mwanga afisa wa polisi kwa niaba ya maafisa usafirishaji. Picha zingine zinaonesha matukio yalivyofanyika kwenye zoezi hilo.

Afisa Tarafa wa Nyaishozi, jijini Dar es Salaam, Ndg. Kelvin Berege amekabithi viakisi mwanga (Reflectors) kwa Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wa Kata zote ndani ya Tarafa ya Nyaishozi, kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha makundi mbalimbali ndani ya jamii, juu ya haki na wajibu wa mwananchi kupiga/Kupigiwa kura hapo ifikapo Novemba 27 mwaka huu kwenye zoezi Zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vitongoji na vijiji. Berege alisema Serikali za mitaa ndiyo sauti ya wananchi, na kuwataka kujitokeza na kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Leave a Comment