×

Wasimamizi Waaswa Kusimamia Viapo Vyao Kuelekea Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa 2024

Kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura pamoja na wasimamizi wa vijiji wameapishwa  22.11.2024 pamoja na kupatiwa Semina juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Wasimamizi hao waliweza kupewa mafunzo mbalimbali juu ya utaratibu wa upigaji kura pamoja na kujumlisha pamoja na utangazaji wa matokeo.

Haya yamefanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27.11.2024 ambapo wananchi wa Urambo wataweza kuchagua viongozi watakaosimamia Serikali za Vijiji na Vitongoji.

Ikumbukwe kuwa Urambo inatarajia kufanya uchaguzi ambao utatoa viongozi katika Vijiji 59 vyenye vitongoji 256 katika kata zote 18.

Aidha Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine anaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wa Urambo kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura tarehe 27.11.2024 ili tusipoteze haki ya kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo.

“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”

SIMULIZI NGUMU SAA 72 CHINI ya KIFUSI SIMU ya RC ILIMPA MATUMAINI-ALIYEMUUA MKWEWE AACHA..

Leave a Comment