×

Rais Mwinyi Ashiriki Maziko Ya Mama mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Maziko ya Bi Mtumwa Ali Salum , Mama mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum.

Maziko hayo yamefanyika kijijini Kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Awali Alhaj Dk.Mwinyi alijumuika na Waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti Msikiti wa Mame Ali Saateni iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih.

Marehemu Bi. Mtumwa Amefariki wakati akitibiwa Katika Hospitali ya Rufaa ya Lumumba alikolazwa.

Rais Alhaj Dk.Mwinyi Ijumaa ya wiki iliyopita aliwahi kumjulia hali Marehemu Bi.Mtumwa Hospitalini hapo.

 

Leave a Comment