
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kujipima ya darasa la nne na kidato cha pili ambapo matokeo ya jumla yanaonesha kuongezeka kwa ufaulu kwa mitihani hiyo.
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2024
Akitangaza matokeo ya darasa la nne, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) Dk Said Mohammed amesema wanafunzi 1,320,227 kati ya 1,530,805 wenye matokeo sawa na asilimia 86.24, wamefaulu kuendelea na darasa la tano mwaka 2025 kwa kupata madaraja A,B,C na D.
Amesema matokeo hayo ni tofauti na mwaka 2023 ambao wanafunzi waliofaulu walikuwa 1,287,934 sawa na asilimia 83.3.4, hivyo kuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.9 kwa wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na darasa la tano ikilinganishwa na mwaka 2023.
Dk Mohamed amesema kati ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na darasa la tano, wasichana ni 699,901 sawa na asilimia 87.75 na wavulana ni 620,326 sawa na asilimka 84.61.
Kwa matokeo hayo, amesema kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, wasichana ni 367,457 na wavulana ni 313,117.