
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imekusudia ya awamu ya sita itaendelea kuboresha huduma za mbalimbali za kiuchumi na kijamii zikiwemo huduma za uhamiaji nchini kuharskisha maendeleo ya watu.
Dkt. Biteko amesema hayo Januari 11, 2025 baada ya Kuweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Uhamiaji Wilaya ya Micheweni, Pemba ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar hatakayofikia kilele Januari 12, 2025.
Amesema Wazanzibari na Watanzania wana kila sababu ya kujivunia maendeleo yaliyopatikana katika kioindi cha miaka 61 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo miradi mbalimbali imetekekezwa ikilinganishwa na kipindi kilichopita.

“ Mtakubaliana na mimi kwamba Serikali zote mbili zinaendelea kufanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Maendeleo haya ni matunda ya Viongozi na waasisi Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere,” Amesema Dkt. Biteko.
Amesema ujenzi wa Afisi na Makaazi ya watumishi wa idara ya Uhamihaji ni ushahidi kwamba Serikali imenuia kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa tija.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Khatib amemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi mingi na mikubwa ya maemdeleo sambamba na kuimarisha demokrasia.
Amesema wakati Wazanzibari wakiendelea kujivunia faraja zinazotokana na Mapinduzi ni muhimu Wananchi kujua na kufahamiana ili kulinda usalama wa nchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamza Hassan Juma amesema maboresho yanayoendelea Wilaya ya Micheweni yamewaondoa katika hali ya umasikini .
Amesema uboreshaji wa miundombinu ya barabara na maji utachochea upatikanaji wa ajira kwa wakazi na hivyo kukuza uchumi na maendeleo.
