×

CCM Yatoa Maazimio ya Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa maazimio ya kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 5 Novemba 2025, kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Laban Kihongosi, kikao hicho kilijadili hali ya kisiasa nchini kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, na kufikia maazimio kadhaa, ikiwemo Kamati Kuu kuwapongeza wananchi wote wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuonesha imani kubwa kwa Chama hicho

Aidha, Kamati Kuu ya Chama hicho imelaani vitendo vya kihuni na uvunjifu wa amani vilivyofanywa na baadhi ya watu na kusababisha vifo pamoja na uharibifu wa mali za umma na za wananchi.

Taarifa imeeleza zaidi kuwa CCM imeazimia kujitathmini na kujiandaa vyema kubeba dhamana ya kuliongoza Taifa, huku kikitoa wito kwa Serikali kuchukua hatua stahiki kuhakikisha nchi inabaki katika hali ya amani na utulivu.

Leave a Comment