×

Trump Aongeza Presha Kwa Iran, Aipa Saa 48 Kufungua Hormuz

 

Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza presha katika mvutano unaoendelea kati ya Marekani na Iran baada ya kuipa Iran muda wa saa 48 kufikia makubaliano au kufungua Mlango wa Hormuz, huku akionya kuwa hatua kali zitachukuliwa endapo haitatii.

Kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wake wa Truth Social, Trump alisisitiza kuwa muda uliobaki ni mfupi na kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua za kijeshi ikiwa Iran itaendelea kukaidi maelekezo hayo. Alieleza kuwa “muda unaisha” na akahimiza upande wa Iran kufanya uamuzi wa haraka ili kuepusha ongezeko la mgogoro.

Hii si mara ya kwanza kwa Trump kutoa onyo la aina hiyo, kwani katika siku za hivi karibuni amekuwa akitoa matamko kadhaa yanayohusiana na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Iran, ikiwa ni sehemu ya shinikizo la kuilazimisha nchi hiyo kukubaliana na masharti yanayowekwa na Marekani.

Mvutano huu unaendelea kuibua wasiwasi wa kimataifa, hasa kutokana na umuhimu wa Mlango wa Hormuz katika usafirishaji wa mafuta duniani, ambapo hatua yoyote ya kuufunga au kuzuia matumizi yake inaweza kuwa na athari kubwa kiuchumi na kisiasa katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Leave a Comment