×

Makonda Awasili Bungeni Akiambatana na Nyota wa Soka Didier Drogba

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda akiwa pamojana mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Klabu ya Chelsea, Didier Drogba wakiwasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, tayari kwa kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2026/27, leo Mei 04, 2026

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, leo Mei 4, 2026 amewasili katika viwanja vya Bunge la Tanzania jijini Dodoma akiwa pamoja na gwiji wa soka wa Ivory Coast, Didier Drogba.

Drogba, ambaye anajulikana sana kwa mafanikio yake akiwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea F.C., alihudhuria tukio hilo maalum ambapo Makonda alikuwa akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Uwepo wa Drogba unaashiria umuhimu wa michezo kimataifa na mchango wake katika diplomasia ya kijamii na maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

AUAWA na KUKATWA KICHWA – MWILI WAOKOTWA MTO MSIMBAZI DAR – POLISI WATOA TAARIFA WAANZA UCHUNGUZI…

Leave a Comment