×

Barcelona Yatwaa Ubingwa wa LaLiga Baada ya Kuifunga Real Madrid El Clasico

FC Barcelona imetwaa ubingwa wa La Liga kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid CF, katika mchezo wa El Clasico uliopigwa kwenye dimba la Camp Nou.

Barcelona imeandika historia kwa kutwaa taji hilo la 29 la LaLiga kwa namna ya kipekee, kwani ni mara ya kwanza bingwa wa ligi hiyo kupatikana rasmi kupitia mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.

Katika mchezo huo, Marcus Rashford aliifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 9 kabla ya Ferran Torres kuongeza bao la pili dakika ya 18 na kuzima matumaini ya Real Madrid.

Matokeo Kamili:
FT: Barcelona 2-0 Real Madrid
⚽ 09’ Rashford
⚽ 18’ Torres

Ushindi huo umeifanya Barcelona kuendelea kutawala soka la Hispania huku mashabiki wao wakisherehekea ubingwa mwingine mkubwa mbele ya wapinzani wao wa jadi.

#PART 2: UNDANI wa USHAHIDI ULIOMTIA HATIANI ‘MR BLUE’ na KUHUKUMIWA KUNYONGWA kwa KUMUUA EZENIA

Leave a Comment