×

DStv Yazindua Kampeni Kubwa ya Kombe la Dunia 2026 Tanzania

Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo.

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma yake ya DStv leo Mei 11, 2026 imezindua rasmi kampeni maalum kuelekea mashindano ya FIFA World Cup 2026, huku ikiahidi kuwaletea Watanzania burudani ya kiwango cha juu kupitia matangazo ya moja kwa moja ya mechi zote za michuano hiyo mikubwa duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, amesema Kombe la Dunia ni tukio kubwa zaidi la michezo duniani kutokana na idadi kubwa ya watazamaji wake duniani kote.

Amesema katika mashindano ya mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni tano walifuatilia michuano hiyo, jambo linalodhihirisha ukubwa na mvuto wa Kombe la Dunia kwa mashabiki wa soka duniani.

“Kombe la Dunia si mashindano ya kawaida. Takwimu zinaonesha watu zaidi ya bilioni tano walifuatilia mashindano ya mwaka 2022, na safari hii tunategemea rekodi hiyo kuvunjwa zaidi,” alisema Shelukindo.

Ameeleza kuwa mashindano ya mwaka 2026 yatakuwa ya kipekee kutokana na kufanyika katika mataifa matatu kwa mara moja ambayo ni United States, Mexico na Canada, huku yakitarajiwa kudumu kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Aidha amebainisha kwamba michuano hiyo itakuwa na ongezeko kubwa la timu kutoka 32 hadi 48, hatua ambayo itazipa nafasi zaidi nchi mbalimbali kushiriki, ikiwemo bara la Afrika ambalo litawakilishwa na jumla ya timu 10.

Kwa upande wa matangazo, amesema chaneli ya SuperSport itaonesha mechi zote 104 za mashindano hayo moja kwa moja, jambo litakalowapa mashabiki nafasi ya kushuhudia kila dakika ya burudani ya soka la dunia.

Katika kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kufuatilia mashindano hayo, kampuni hiyo imekuja na kifurushi maalum cha gharama nafuu cha shilingi 27,500 pekee kitakachowawezesha wateja kutazama mechi zote kwa siku 39 za mashindano.

Pia, MultiChoice Tanzania imetangaza ofa maalum kwa wateja wake ambapo mteja mwenye dish atapata dekoda kwa shilingi 15,000 tu, huku ambaye hana vifaa kamili akiweza kupata kifurushi kizima kwa shilingi 45,000.

MultiChoice Tanzania Yazindua Kampeni Maalum ya Kombe la Dunia 2026

Leave a Comment