×

Rais Samia Aongoza Mazungumzo na Putin Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Urusi Vladmir Putin pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow, tarehe 03 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, yaliyofanyika katika Ikulu ya Kremlin jijini Moscow, Urusi, tarehe 03 Juni 2026.

Mazungumzo hayo yalihusisha masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi, biashara, uwekezaji pamoja na maendeleo katika sekta muhimu zikiwemo nishati, elimu na teknolojia.

Ziara hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Urusi, huku viongozi hao wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika maeneo yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Mbali na mazungumzo hayo, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimataifa pamoja na mikutano ya kiuchumi inayofanyika nchini humo.

Rais Samia akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Urusi Vladmir Putin katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow, tarehe 03 Juni, 2026.
Rais Samia akiwasili katika Ikulu ya Kremlin jijini Moscow.


Leave a Comment