×

Helikopta ya Kijeshi ya Marekani Yaanguka Hormuz, Trump Afunguka

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa wanajeshi wawili wa helikopta ya kijeshi ya Marekani wako salama baada ya kuokolewa katika Mlango Bahari wa Hormuz, eneo linalodhibitiwa kwa sehemu na Iran.

Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Marekani helikopta aina ya Apache ilianguka baharini, na baadaye droni ya majini ya Jeshi la Marekani iliwapata na kuwaokoa Wanajeshi  wake wawili ndani saa mbili. Wote walikuwa katika hali nzuri.

Hata hivyo, bado haijafahamika chanzo cha ajali hiyo ikiwa ni mashambulizi, hitilafu ya kiufundi, au sababu nyingine. Trump amesema taarifa kamili itatolewa baadaye.

Tukio hilo linatokea wakati hali ya mvutano kati ya Iran na Israel ikianza kupungua baada ya pande zote mbili kukubali kusitisha mashambulizi kufuatia wito wa Trump.

MBUNGE SHIGONGO AMLIZA MAMA ALIYEMWAMBIA AENDE BENKI AKACHUKUE PESA – ASEMA ALIDHANI UTANI…

Leave a Comment