
KAMPUNI ya uzalishaji wa mikate na vitafunwa mbalimbali ya Royal Oven yenye makao yake makuu jijini Mwanza na matawi yake jijini Dodoma na kwingineko imetunukiwa cheti cha ubora wa bidhaa zao na shirika la ubora wa viwango nchini TBS.

Kampuni hiyo imetukiwa cheti hicho makao makuu ya TBS jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita ambapo sasa bidhaa zao zitakuwa na nembo ya TBS baada ya kukidhi ubora wa viwango.

Akizungumza na Global Tv baada ya kukabidhiwa cheti hicho Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Mwanabure Ihuya amesema kwa muda mrefu walikuwa wakipambania ubora katika bidhaa zao mpaka TBS nayo ikawaona na kuwatunukia cheti hicho.


“Huu ni mwanzo tu wa ndoto zetu ambapo tunataka kufanya bora zaidi ya hapa kwani hata hapa tulipofikia ni malengo ya muda mrefu.
“Kwa cheti hiki ambacho tulikiwania kwa zaidi ya miaka tisa sasa kimetupa hamasa ya kuzidi kupiga kazi na kuboresha bidhaa zetu na tunawaomba wateja wetu wazidi kutuamini” alisema Mkurugenzi Mwanabure.
Kwa mawasiliano zaidi na Royal Oven wanapatikana katika mitandao yao ya kijamii,
instagram: royaloven mwanza
facebook: royalovendodoma