
Juni 10 2026- Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania leo Juni 10, 2026 imeendesha zoezi la la uchangiaji damu wa hiari kitaifa kwa kushirikiana na taasisi ya Taifa ya Mpango wa Damu Salama (NBTS).

Zoezi hilo lililofanyika katika mikoa sita ya Tanzania ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya, Tabora na Mtwara ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 11 ya ushirikiano wao unaolenga kuhamasisha na kusaidia juhudi za ukusanyaji wa damu nchini ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya upungufu wa damu katika hospitali na vituo vya afya nchini.

Kwa zaidi ya miaka kumi sasa benki ya Exim Tanzania na taasisi ya Taifa ya Mpango wa Damu Salama (NBTS) wamekuwa wakishirikiana kuhamasisha wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi. Zaidi ya chupa 800 za damu zinayokusanywa kila mwaka, kupitia kampeni hizi zimekuwa zikisaidi Benki ya Taifa ya Damu Salama kuwa na akiba ya kutosha ya kuokoa maisha ya kina mama wanaopata changamoto wakati wa kujifungua, waathirika wa ajali, wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji, watoto na wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu kutokana na hali mbalimbali za kiafya.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua kampeni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Benki ya Exim jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania Kauthar D’souza amesema kampeni hii ya uchangiaji wa Damu inaonyesha dhamira ya kudumu ya benki katika kusaidia vipaumbele vya afya ya taifa huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa.
“Benki ya Exim, tunaamini kuwa jukumu letu sio kutoa huduma za kifedha pekee, bali kuwa muhimu mshirika wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Kupitia programu yetu ya Exim Cares, tunaendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, ubunifu, uhifadhi wa mazingira na uwezeshaji wa jamii ili kuleta mabadiliko chanya na endelevu”. Amesema Kauthar
“Kampeni hii ya uchaguaji wa damu ni mfano wa namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na taasisi za umma katika kutatua changamoto zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Ninatoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa za kuchangia damu kujitokeza na kushiriki katika kampeni hii. Dakika chache za muda wako zinaweza kuokoa maisha ya mtu mwingine. Mchango wako unaweza kuwa sababu ya mama kurudi salama kwa familia yake, mtoto kupata matibabu anayohitaji au mgonjwa kupewa nafasi nyingine ya kuendelea kuishi”. Ameongeza Kauthar
Akizungumza kwa niaba ya taasisi ya Taifa ya Mpango wa Damu Salama (NBTS), Afisa Uhamasishaji Damu Salama Kanda ya Mashariki Evelyn Dielly ameipongeza Benki ya Exim kwa ushirikiano wake endelevu na mchango wake katika kuimarisha juhudi za ukusanyaji damu nchini.
“Tunathamini sana msaada unaoendelea kutolewa na Exim Bank kwa miaka mingi. Ushirikiano kama huu ni muhimu katika kusaidia kuongeza uelewa kuhusu uchangiaji wa damu wa hiari na kuimarisha upatikanaji wa damu kwa wagonjwa kote nchini. Kila chupa moja ya damu inayokusanywa husaidia kuokoa maisha ya mgonjwa pamoja vituo vya afya kukabiliana na mahitaji ya dharura ya kitabibu”. Amesema Evelyn
Kampeni hii ya kila mwaka iliyodumu kwa miaka kumi na moja, inadhihirisha ushirikiano wa dhati kati ya Benki ya Exim Tanzania na NBTS, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza utamaduni wa uchangiaji damu wa hiari nchini Tanzani