
Mchezo huu una umuhimu wa kihisia kwa Nigeria, kwani wanakumbwa na kumbukumbu ya kipigo cha 4-0 walichopokea kutoka kwa Portugal mnamo Novemba 2022, kabla ya Kombe la Dunia Qatar.
Tofauti kubwa ni kwamba katika mechi hiyo ya awali, nyota wa dunia Cristiano Ronaldo hakucheza kutokana na ugonjwa wa gastritis, lakini leo nahodha huyo wa Al Nassr anatarajiwa kuvaa jezi la Portugal kwa mara ya kwanza dhidi ya Super Eagles akiwa na umri wa miaka 41. Uwanja wa mechi ni Estádio Dr. Magalhães Pessoa mjini Leiria, na Portugal inaiona mechi hii kama jitihada za mwisho kabla ya kuondoka kwenda Amerika Kaskazini kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026.
Kocha Roberto Martínez ameita kikosi chenye nguvu zaidi akijumuisha Ronaldo anayemaliza msimu mzuri Saudia, Bruno Fernandes anayeshikilia rekodi ya pasi za kufunga zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza, na Bernardo Silva anayesimamia ubunifu wa kati. Mabadiliko makubwa kwenye safu ya ushambuliaji ni pamoja na Gonçalo Ramos na João Félix ambao wana uwezo wa kuingia na kubadilisha mchemo kutoka benchi. Portugal ina rekodi nzuri dhidi ya Nigeria, na ushindi wa 4-0 mwaka 2022 unawapa kujiamini, lakini wamekuwa wakikosa uthabiti kwenye michezo ya ugenini hivi karibuni, hasa wanapokabiliwa na timu zenye kasi ya mashambulizi.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Super Eagles wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na morali iliyoinuka kutokana na sare ya 2-2 dhidi ya Poland, ambapo walionyesha uwezo wa kutawala mchezo lakini walighafilika dakika za mwisho. Alex Iwobi na Samuel Chukwueze wamejiunga na kambi Lisbon baada ya kukosa mechi ya Poland, huku beki mwenye umri wa miaka 21, Christian Akpan akipata wito wa kwanza kwenye kikosi
Eneo la kati utakuwa uwanja wa vita kuu, kwani Bruno Fernandes anayetambulika kama mtoa pasi bora wa Ligi Kuu atakutana na Wilfred Ndidi anayejulikana kwa uwezo wake wa kukaba na kuvunja mashambulizi. Mchezo huu utakuwa wa kihistoria kwani ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kucheza dhidi ya Nigeria, na anatafuta kuongeza idadi yake ya mabao ya kimataifa. Kwa upande wa Nigeria, Paul Onuachu aliyefunga penalti dhidi ya Poland na Terem Moffi ndio wanaotarajiwa kuongoza safu ya ushambulaji, wakitegemea pasi za ubunifu kutoka kwa Alex Iwobi atakayecheza nafasi ya kiungo wa kati.
Kocha Eric Chelle anatarajiwa kutumia mfumo wa 4-4-2 au 3-4-3 unaosisitiza mashambulizi ya haraka, kama alivyoonesha dhidi ya Poland, huku Calvin Bassey na Abdullahi Bewene wakiwa ni funguo katika safu ya ulinzi.
Portugal itapendelea kumiliki mpira kwa kina na kutumia wapana Nuno Mendes na João Cancelo kushambulia kutoka pembeni. Licha ya kujiamini kwa Nigeria, ubora wa Portugal unatarajiwa kushinda, lakini ikiwa Super Eagles wataweza kuzuia mashambulizi ya mapema na kutumia wapiga kasi wao kama Chukwueze, wanaweza kutoa mshangao.