
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza nafasi 85 za kazi katika taasisi mbalimbali za umma nchini, ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), Makumbusho ya Taifa Tanzania (NMT) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Tangazo hilo lililotolewa Juni 13, 2026, linatoa fursa kwa Watanzania wenye sifa stahiki kuomba nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti, diploma, shahada hadi shahada za uzamili katika kada tofauti.
Soma zaidi hapa >>> NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
Miongoni mwa nafasi zilizotangazwa ni Mwalimu wa Hisabati na Sayansi, Artisan II, Laboratory Assistant, Audiologist, Audiometrist, Radiotherapist, pamoja na nafasi za wahadhiri wasaidizi na wasaidizi wa kufundisha katika fani mbalimbali ikiwemo Sheria, ICT, Saikolojia, Uhasibu, Jamii na Mazingira.
Aidha, TASAC imetangaza nafasi tisa za Flag and Port State Control Officer II, huku NMT na TAWIRI zikihitaji wataalamu wa utafiti, uhifadhi wa urithi wa taifa, zoolojia, botania, usimamizi wa wanyamapori na tiba za mifugo.
PSRS imeeleza kuwa waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania na kutuma maombi yao kupitia mfumo wa Ajira Portal pekee. Waombaji pia wanatakiwa kuambatanisha vyeti vyao vilivyothibitishwa pamoja na nyaraka nyingine muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo.
Mwisho wa kupokea maombi ni Juni 26, 2026, huku waombaji watakaokidhi vigezo pekee wakitarajiwa kuitwa kwenye usaili.
Sekretarieti hiyo imeonya kuwa uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa za uongo utachukuliwa hatua za kisheria, na kusisitiza kuwa maombi yote yatakayowasilishwa nje ya mfumo rasmi wa Ajira Portal hayatapokelewa.
Mwisho wa kutuma maombi ni Juni 26, 2026