×

Kutoka Marekani: Patricia Asimulia Kifo Kilivyomsogelea – Video

Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Ajuna Ishemo (Patricia), amefunguka kuhusu maisha yake na mtoto wake, akieleza jambo la kushangaza la kiimani kuhusu mwanawe kuwa na karama ya kuota ndoto ambazo hutimia.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mtangazaji na mtumishi wa Mungu Lillian Mwasha akiwa nchini Marekani, Patricia amesema mwanawe amekuwa akipata ndoto mbalimbali ambazo baadaye huja kutokea katika uhalisia. Amesema hata mazingira ya maisha yao ya sasa na sehemu wanayoishi, mwanawe aliwahi kuyaota kabla ya kuyafikia.

Patricia ameeleza kuwa jambo hilo limempa mshangao mkubwa lakini pia limemjenga kiimani, akiamini kuwa ni moja ya karama maalum ambazo zinahitaji uangalizi na maombi. Ameongeza kuwa safari yake ya kuishi Marekani haikuwa rahisi, lakini kupitia uvumilivu na imani amefanikiwa kujenga maisha mapya.

Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi wakionyesha kushangazwa na madai hayo ya ndoto kutimia, huku wengine wakisema ni jambo la kawaida la kisaikolojia au bahati ya matukio kufanana.

Leave a Comment