×

Fahamu Mabilionea 10 Matajiri Zaidi Duniani Mwaka 2026

Dunia inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa utajiri wa viongozi wa sekta ya teknolojia, huku orodha ya mabilionea matajiri zaidi mwaka 2026 ikitawaliwa na wafanyabiashara waliowekeza katika teknolojia, akili bandia (AI), biashara mtandaoni na huduma za kidijitali.

Kinara wa orodha hiyo ni Elon Musk, ambaye ameandika historia kwa kuwa mtu wa kwanza kufikisha utajiri unaokadiriwa kuzidi dola trilioni moja, akichochewa na mafanikio ya kampuni zake za Tesla, SpaceX na xAI.

Nafasi ya pili na ya tatu zinashikiliwa na waanzilishi wenza wa Google, Larry Page na Sergey Brin, ambao wameendelea kunufaika na ukuaji wa biashara za teknolojia na akili bandia.

Mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos, anashika nafasi ya nne, akifuatiwa na mwanzilishi wa Oracle, Larry Ellison, huku Michael Dell wa Dell Technologies akishika nafasi ya sita.

Mwanzilishi wa Meta, Mark Zuckerberg, ameendelea kubaki miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kutokana na mafanikio ya kampuni yake inayomiliki Facebook, Instagram na WhatsApp.

Katika nafasi ya nane yupo Jensen Huang, ambaye ameshuhudia ongezeko kubwa la utajiri wake kutokana na mafanikio ya NVIDIA katika soko la chips za akili bandia.

Mfaransa Bernard Arnault ndiye tajiri mkubwa zaidi kutoka sekta ya bidhaa za anasa, huku mwekezaji mkongwe Warren Buffett akifunga orodha ya matajiri 10 bora duniani.

Mabilionea 10 Matajiri Zaidi Duniani 2026

  1. Elon Musk – Dola trilioni 1.3
  2. Larry Page – Dola bilioni 301.4
  3. Sergey Brin – Dola bilioni 277.9
  4. Jeff Bezos – Dola bilioni 255.5
  5. Larry Ellison – Dola bilioni 241.4
  6. Michael Dell – Dola bilioni 231.2
  7. Mark Zuckerberg – Dola bilioni 203.8
  8. Jensen Huang – Dola bilioni 183.6
  9. Bernard Arnault – Dola bilioni 159.2
  10. Warren Buffett – Dola bilioni 146.4

Orodha hiyo inaonyesha jinsi sekta ya teknolojia na akili bandia zinavyoendelea kuzalisha utajiri mkubwa duniani, huku wafanyabiashara waliowekeza katika ubunifu wa kidijitali wakiongoza kwa mbali miongoni mwa matajiri wakubwa wa dunia.

Leave a Comment