
Nyota wa muziki wa pop duniani, Justin Bieber, ameendelea kujijengea umaarufu mkubwa si tu kupitia muziki bali pia kupitia utajiri mkubwa unaotokana na kazi yake ya muda mrefu katika tasnia ya burudani.
Katika kipindi cha miaka yake ya mafanikio, Bieber amekusanya mali mbalimbali za thamani kubwa ikiwemo mauzo ya katalogi yake ya nyimbo 291, ambayo iliripotiwa kumuingizia takribani dola milioni 188 mwaka 2022. Pia ziara yake kubwa ya “Purpose World Tour” ilizalisha zaidi ya dola milioni 193 kupitia mauzo ya tiketi.
Mbali na muziki, Bieber anamiliki majumba ya kifahari ikiwemo shamba lake la La Quinta California lenye thamani ya dola milioni 16.4 pamoja na nyumba ya ziwani Ontario yenye thamani ya takribani dola milioni 5. Pia anamiliki ndege binafsi aina ya Gulfstream G600 yenye thamani ya karibu dola milioni 60 pamoja na basi la kifahari la ziara lenye thamani ya takribani dola milioni 2.

Katika upande wa magari, Justin Bieber anajivunia mkusanyiko wa magari ya kifahari ikiwemo Lamborghini Aventador iliyobadilishwa maalum yenye thamani ya takribani dola 500,000 pamoja na Ferrari 458 Italia yenye thamani ya zaidi ya dola 434,000.
Pia katika maisha yake binafsi, Bieber aliwahi kumzawadia mke wake, Hailey Bieber, pete ya uchumba ya almasi ya karati 10 yenye thamani inayokadiriwa kufikia dola 500,000.
Kwa ujumla, safari ya Justin Bieber kutoka kuwa kijana aliyegunduliwa mapema hadi kuwa mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa zaidi duniani inaakisi mafanikio makubwa ya kifedha na maisha ya kifahari aliyonayo leo.




