
SERIKALI imesema kuwa imedhamiria kuhakikisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Indonesia unaleta matokeo kwa kuongeza thamani ya biashara kati ya nchi hizo.
Hayo ameyasema kwenye maonesho ya 50 ya sabasabaDar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa TANTRADE, Prof, Ulingeta Mbamba alipokuwa akizungumza katika hafla ya Siku ya Indonesia kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Alisema Indonesia imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na maendeleo ya viwanda, usindikaji wa mazao ya uvuvi, teknolojia za kilimo cha majini, mavazi, bidhaa za matumizi ya kila siku, sekta ya nishati na maendeleo ya viwanda kwa ujumla. huku Tanzania ikiwa na fursa nyingi katika sekta za madini, utalii, uchumi wa buluu, viwanda na maendeleo ya miundombinu.
Alieleza kuwa sekta hizo zinatoa msingi imara wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Serikali, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, ina dhamira ya kuhakikisha ushirikiano huu unazaa matokeo chanya kwa kuongeza thamani ya biashara kati ya nchi zetu, kuhamasisha ubia katika uwekezaji, kuimarisha matumizi ya teknolojia na maarifa, pamoja na kusaidia ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni za Tanzania na Indonesia,” ameeleza
Amesema Tanzania inatarajia kuona biashara kati ya nchi hizo ikiendelea kukua kwa uwiano, ambapo bidhaa nyingi zaidi kutoka Indonesia zitapata soko nchini na bidhaa nyingi zaidi za Tanzania zitaingia na kufikia soko la Indonesia.
“Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) zimejizatiti kuendeleza maendeleo ya viwanda, kuboresha mazingira ya biashara, kuhamasisha uongezaji thamani, kupanua fursa za mauzo ya nje na kujenga mazingira wezeshi yanayochochea ukuaji wa biashara,” aliongeza.

Akizungumzia maonesho ya Sabasaba yanayoendelea amesema
tangu kuanza kwake, yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonesha uwezo wa Tanzania kuvutia uwekezaji na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na washirika wa maendeleo.
“Ushiriki endelevu wa Indonesia katika maonesho haya kwa miaka mitatu mfululizo unastahili pongezi za dhati. Ushiriki huo unaonesha si tu imani waliyonayo katika jukwaa hili, bali pia nia yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa biashara na uchumi kati ya Tanzania na Indonesia,” ameafanua.
Kwa Upande wake Naibu Balozi wa Indonesia Priadji Soelaiman Naibu Balozi wa amesema Indonesia na Tanzania ina mashirikino ya mda mrefu katika kiplomasia hivyo kuwa na tija Katika kuchechemua Uchumi.