×

Mexico Warejesha Saa za Rolex Baada ya Sheria za FIFA

Timu ya taifa ya Mexico imelazimika kurejesha saa za kifahari za Rolex zilizotolewa na content creator maarufu Steve Will Do It, baada ya kubainika kuwa zawadi hizo zinaweza kwenda kinyume na kanuni za maadili za FIFA.

Kwa mujibu wa taarifa, Deleonardis alisema alitumia takribani dola milioni 1 kununua saa hizo kwa kila mchezaji na baadhi ya viongozi wa timu hiyo, akizikabidhi wakati alipokutana na kikosi hicho kabla ya mechi yao ya hatua ya 16 bora.

Hata hivyo, sheria za FIFA kupitia Kanuni ya Maadili zinakataza wachezaji na viongozi kukubali zawadi zenye thamani kubwa, zikisema kuwa zawadi zinapaswa kuwa za thamani ya kawaida au za kiishara tu.

Kutokana na masharti hayo, Mexico ilithibitisha kupitia akaunti yao ya X kwamba saa hizo zilirejeshwa kwa makubaliano ya pande zote, huku zikielezwa kuwa zilikuwa zawadi binafsi kutoka kwa SteveWillDoIt bila mpango rasmi wa shirikisho.

Tukio hilo linajiri wakati Mexico ikiendelea na harakati zake katika Kombe la Dunia 2026, wakilenga kufikia robo fainali kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1986 walipokuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Leave a Comment