
Tanasha Donna, mama wa mtoto wa msanii wa Tanzania Diamond Platnumz, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa Julai 7, 2026 huku akitoa shukrani kwa Mungu kwa kufikisha mwaka mwingine wa maisha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha aliandika ujumbe mfupi wa kushukuru akisema:
“Chapter 31! Alhamdulillah for another year. ♥️🎂🎉”
Ujumbe huo uliambatana na emoji za shangwe na upendo, huku mashabiki wake wakimiminika kumtakia heri na mafanikio zaidi katika mwaka wake mpya wa maisha.
Tanasha Donna amekuwa akijulikana katika ukanda wa Afrika Mashariki kupitia kazi zake za muziki, uanamitindo na shughuli mbalimbali za burudani, huku pia akifuatiliwa sana kutokana na historia yake ya mahusiano na Diamond Platnumz.
