
Rais wa Marekani Donald Trump leo Julai 13, 2026 amedai kuwa viongozi wakuu wa kijeshi wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa uwezo wa kijeshi wa taifa hilo umeathirika kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika mahojiano na Fox News, Trump alisema Iran imepoteza uwezo wake wa kijeshi katika maeneo muhimu, akidai vikosi vyake vya anga na majini pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga vimeharibiwa.
“Hawana jeshi la majini, hawana jeshi la anga, yote yameondoka. Mifumo yao ya ulinzi wa anga imeharibiwa, viongozi wao wote wameuawa, viongozi wao bora wameuawa,” alisema Trump.
Trump pia alitoa kauli kuhusu Mojtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran, akisema:
“Khamenei ameondoka, na mwanawe yuko asilimia 90.”
Hata hivyo, Trump hakutoa maelezo zaidi kuhusu kauli hiyo wala ushahidi wa kuthibitisha madai yake. Kufikia sasa, mamlaka za Iran hazijatoa tamko rasmi kujibu kauli hizo.