×

Mahakama Kuu Yafuta Kesi ya Kupinga Ushindi wa Ubunge wa Baba Levo Jimbo la Kigoma Mjini

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Kigoma, imeifuta kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Jimbo la Kigoma Mjini yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Levocatus Chipando, maarufu Baba Levo.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi, Julai 16, 2026, na Jaji Victoria Nongwa, ambaye amesema ushahidi uliowasilishwa na walalamikaji haukufikia kiwango cha kuwalazimisha walalamikiwa kujibu madai yaliyokuwa yamewasilishwa dhidi yao.

Kesi hiyo ya uchaguzi namba 28949 ya mwaka 2025, ilitokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, na ilifunguliwa na wananchi wanne wanaojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini.

Waliofungua kesi hiyo ni Johary Kabourou, Luma Akilimali, Pendo Kombolela na Lumu Mwitu, wakipinga matokeo yaliyomtangaza Baba Levo kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu, kesi hiyo imehitimishwa baada ya mahakama kuridhika kuwa ushahidi uliotolewa haukutosha kuendelea na hatua ya utetezi kutoka kwa walalamikiwa.

Leave a Comment