×

Netanyahu Atangaza Kuishabikia Argentina Dhidi ya Hispania Fainali

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ametangaza wazi kuipa sapoti Argentina kuelekea fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kukabidhiwa jezi rasmi ya timu hiyo na Balozi wa Argentina nchini Israel, Rabbi Shimon Axel Wahnish.

Katika video iliyotolewa Jumamosi, Wahnish alimkabidhi Netanyahu jezi hiyo huku akitania kwa Kiebrania kwamba ilikuwa jezi ya mwisho iliyobaki kutokana na zote kuuzwa.

Baadaye, Wahnish alimchezea Netanyahu ujumbe wa sauti kutoka kwa Rais wa Argentina, Javier Milei, aliyemshukuru kwa kuiunga mkono Argentina na kueleza kufurahishwa na uamuzi wake wa kuisapoti timu hiyo katika mchezo wa fainali.

Akizungumza baada ya kupokea jezi hiyo, Netanyahu alisema hafichi kwamba ni shabiki wa Argentina, akiongeza kuwa Waisraeli wengi pia wanaunga mkono timu hiyo.

“Sifichi kwamba mimi ni shabiki wa Argentina, na naamini wananchi wengi wa Israel pia ni mashabiki wao. Hiyo ni kwa sababu Rais Milei ameleta mageuzi makubwa katika uhusiano kati ya Israel na Argentina. Hatuna marafiki wakubwa na bora zaidi kuliko wao, ndiyo maana tunawaunga mkono,” alisema Netanyahu.

Argentina itavaana na Hispania katika fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa Jumapili.

Leave a Comment