
Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji chipukizi Juma Issa Abushuri, maarufu kama Chuga Boy, kuwa mchezaji mpya wa timu hiyo baada ya kumsajili akitokea Fountain Gate FC.
Chuga Boy anakuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga katika dirisha kubwa la usajili la msimu wa 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi yanayofanywa na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Usajili huo unaonyesha dhamira ya Yanga ya kuendelea kuimarisha safu yake ya ushambuliaji na kuongeza ushindani ndani ya kikosi, huku mashabiki wakitarajia kuona kiwango kitakachomfanya Chuga Boy kung’ara akiwa katika jezi ya kijani na njano.

