×

Mashabiki Wamzomea Donald Trump Kabla ya Kukabidhi Kombe la Dunia 2026

Rais wa Marekani, Donald Trump, alizomewa na sehemu ya mashabiki waliohudhuria fainali ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Hispania na Argentina, aliposhuka uwanjani kushiriki hafla ya kukabidhi medali na kombe baada ya mchezo huo.

Trump alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria mechi hiyo iliyofanyika Julai 19 katika Uwanja wa New York New Jersey, ambapo Hispania ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Argentina bao 1-0 kupitia bao la Ferran Torres lililofungwa dakika ya 106 ya muda wa nyongeza.

Baada ya mechi kumalizika, Trump aliongozana na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kwenda uwanjani kuwapongeza na kuwakabidhi medali wachezaji wa timu zote mbili. Hata hivyo, alipoonekana uwanjani, sauti za kuzomea zilisikika kutoka kwa baadhi ya mashabiki waliokuwepo, huku Trump akiwapungia mkono mashabiki hao.

Katika mechi hiyo, Trump alikuwa ameketi katika eneo maalumu la wageni wa heshima akiwa na Mke wake Melania Trump, mwanawe Eric Trump, mjukuu wake Barron Trump, pamoja na viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sánchez, Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum, Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Hispania.

Kabla ya mchezo kuanza, Trump aliizungumza na Fox Sports na kusema mafanikio ya Kombe la Dunia nchini Marekani yameonyesha kuwa taifa hilo sasa ni moja ya mataifa makubwa ya soka.

Hata hivyo, uhusiano wake na mashabiki wa soka uliibua mjadala mapema katika mashindano hayo baada ya kuripotiwa kumpigia simu Rais wa FIFA, Gianni Infantino, akiomba kadi nyekundu aliyopewa mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun ipitiwe upya. Adhabu hiyo ilifutwa na Balogun akaruhusiwa kucheza hatua ya 16 bora, jambo lililozua malalamiko kutoka kwa mashabiki wengi wa soka duniani.

Baada ya Marekani kuondolewa na Ubelgiji kwa mabao 4-1, baadhi ya wachezaji wa Ubelgiji walionekana wakimdhihaki Trump kwa kuiga mtindo wake maarufu wa kucheza wakati wa kampeni zake za kisiasa.

Tukio la kuzomewa kwa Trump katika fainali ya Kombe la Dunia limeendelea kuzua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku video za tukio hilo zikisambaa kwa kasi.

Leave a Comment