×

Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga Adai hajui Kama Tundu Lissu Aliwahi Kuwa Rais wa TLS

Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Andrew Shaban, amesema hafahamu kama Tundu Lissu aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Shahidi huyo ametoa kauli hiyo leo, Julai 23, 2026, alipokuwa akihojiwa maswali ya dodoso na Wakili Emmanuel Ukashu wa TLS katika Shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 linaloendelea Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam huku akikiri kuwafahamu waleta maombi watatu kuwa ni mawakili,

Katika ushahidi wake, ACP N’tamamiro alisema kauli ya “maagizo kutoka juu” anaielewa kama maagizo ya kiutendaji kutoka kwa viongozi wake, na kwamba hawezi kubishana nao, ingawa alisisitiza kuwa zipo taratibu za kufuatwa kabla ya hatua yoyote ya kinidhamu. Pia alisema anamfahamu Nashon Nkung na Paul Kisabo kwa kuwa amekuwa akiwaona wakimtembelea Tundu Lissu gerezani, huku akieleza kuwa hajawahi kumuona wala kumfahamu Kulwa William Maduhu.

Baada ya kukamilika kwa maswali ya dodoso na re-examination, Mahakama iliahirisha shauri hilo hadi Septemba 16, 2026, litakapoitwa tena, huku pande zote zikielekezwa kuwasilisha hoja zao kwa maandishi kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na waleta maombi. Shauri hilo linahusu madai ya mawakili wa Tundu Lissu kwamba walinyimwa faragha ya kuzungumza na mteja wao walipokuwa wakimtembelea Gereza la Ukonga, jambo wanalodai linakiuka Katiba pamoja na sheria na taratibu za nchi.

Leave a Comment