
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehutubia Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu afya uliofanyika katika Hoteli ya Elisa, jijini Accra nchini Ghana, Julai 22, 2026.
Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya afya barani, kuongeza uwezo wa kukabiliana na milipuko ya magonjwa, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma bora za afya.
Ushiriki wa Rais Samia unaonesha dhamira ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na mataifa mengine ya Afrika katika kutafuta suluhisho endelevu kwa changamoto za sekta ya afya na kuendeleza ajenda ya afya kwa maendeleo ya bara la Afrika.


