×

Wanafunzi Shule ya Msigi Goba Matosa Wapokea Msaada wa Madawati

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Goba Matosa iliyopo Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam wamepokea msaada wa madawati 23 pamoja na tangi la kuhifadhia maji.
Hiyo ni katika kuendeleza utekelezaji wa programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility (CSR), Fasthub Solutions Ltd imekabidhi madawati 23 pamoja na tanki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa lita 3,000.

Msaada huo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi kwa kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati na kuimarisha upatikanaji wa maji safi kwa matumizi ya kila siku shuleni.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Taasisi hiyo, Christine Abulista amesema: “Tunaamini kuwa kuwekeza katika elimu ni kuwekeza katika mustakabali wa Tanzania. Kila mtoto anastahili kujifunza katika mazingira bora na salama”

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Simon Matemanga ameishukuru Fasthub Solutions Ltd kwa msaada huo, akieleza kuwa madawati yaliyotolewa yatasaidia kupunguza msongamano na changamoto ya uhaba wa madawati madarasani, huku tanki la maji likiimarisha upatikanaji wa maji kwa wanafunzi na walimu.

Leave a Comment