×

Video: Majaliwa Amtembelea Mkubwa Fella, Amkabidhi Msaada wa Milioni 20

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, Julai 25, 2026 amefika nyumbani kwa mdau wa muziki na mlezi wa vipaji nchini, Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella, kwa lengo la kumjulia hali huku akimkabidhi msaada wa shilingi milioni 20.

Katika ziara hiyo, Majaliwa alipata fursa ya kufanya mazoezi mepesi ya viungo pamoja na Mkubwa Fella, ikiwa ni sehemu ya kumpa hamasa na kumtia moyo katika kipindi anachoendelea kuimarisha afya yake.

Mbali na kumjulia hali, wawili hao walifanya mazungumzo kuhusu mchango mkubwa wa Mkubwa Fella katika maendeleo ya muziki wa Tanzania, hususan katika kugundua, kulea na kuendeleza vipaji vya wasanii wengi waliofanikiwa ndani na nje ya nchi.

Pia walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya sekta ya sanaa na burudani nchini, huku Majaliwa akitambua mchango wa Mkubwa Fella katika kukuza tasnia hiyo kwa miaka mingi.

Leave a Comment