
Loo Jumapili, tarehe 9 Agosti 2026, katika uwanja wa Sparta-Stadion Het Kasteel. itapigwa Mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Uholanzi (Eredivisie) kati ya Sparta Rotterdam na Feyenoord majira ya saa 7:15 mchana.
Mechi hii ni maalum kwa sababu ni “derby” ya jiji la Rotterdam, timu mbili zinazotoka mji mmoja lakini zenye historia tofauti kabisa ya mafanikio. Kabla ya mchezo huu, kuna habari muhimu ya kiutawala upande wa Feyenoord, Robin van Persie ameondolewa kwenye nafasi ya kocha mkuu wa Feyenoord, jambo litakaloathiri hali ya kisaikolojia na maandalizi ya timu wakiingia msimu mpya bila uhakika wa uongozi wa benchi.
Kwa upande wa historia ya mechi hizi mbili, takwimu zinaonyesha ubora mkubwa wa Feyenoord. Kati ya mechi 38 zilizowahi kuchezwa kati ya timu hizi, Sparta Rotterdam wameshinda mara mbili tu, Feyenoord wameshinda mara kumi na tano, na mechi nne zimeishia sare.
Hata hivyo, mechi ya mwisho kati yao ilikuwa ya kushangaza kidogo Sparta waliweza kuwavuruga Feyenoord kwa matokeo ya kushangaza mjini kwao mnamo Januari 2026, jambo linaloonyesha kuwa ushindani wa ndani wa jiji mara nyingi hauheshimu takwimu za jumla.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kabla ya mechi hii, Feyenoord walikuwa wakiendelea kupambana na changamoto za majeruhi. Wachezaji kadhaa wa Feyenoord hawapo kwa sababu ya majeraha, akiwemo Anel Ahmedhodzic, Jakub Moder, Leo Sauer, Malcolm Jeng, Thomas Beelen, na Shiloh ‘t Zand. Hii ni orodha ndefu ya majeruhi ambayo inaweza kuathiri sana muundo wa ulinzi na kati ya uwanja wa Feyenoord katika mechi hii ya ufunguzi wa msimu.
Kwa jumla, licha ya ubora wa kihistoria wa Feyenoord, mabadiliko ya uongozi wa kiufundi na majeruhi mengi yanaweza kuwapa Sparta Rotterdam fursa nzuri ya kuwashinda majirani zao mbele ya mashabiki wao wenyewe.