×

UDSM Yatangaza Nafasi 33 za Tutorial Assistant, Maombi Mwisho Agosti 18, 2026

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza nafasi 33 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, kwa ajili ya kujaza nafasi za Tutorial Assistant katika taaluma mbalimbali.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, nafasi hizo zinapatikana katika vitengo na idara mbalimbali za chuo, zikiwemo Sayansi ya Kilimo, Uhandisi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Sayansi za Kompyuta, Fizikia, Sanaa, Masomo ya Jinsia, Masomo ya Maendeleo, Uhasibu, Sayansi za Maji na Uvuvi, Elimu na Sayansi za Afya.

Miongoni mwa nafasi zilizotangazwa ni Tutorial Assistant katika Entrepreneurship and Innovation, Geographic Information Systems, Agricultural Production and Farm Management Economics, Veterinary Medicine, Architecture, Quantity Surveying, Construction Management, Structural Engineering, Transportation Engineering, Geotechnical Engineering na Geomatics Engineering.

Pia kuna nafasi tatu za Tutorial Assistant katika Computer Science katika Kampasi ya Kagera, nafasi mbili za Medical Physics, nafasi mbili za Gender Studies pamoja na nafasi tatu katika Taxation/Public Sector Accounting and Auditing.

Nafasi nyingine ni pamoja na Film and Television, Development Studies, Information Technology, Aquaculture Genetics, Hydrology, Artificial Intelligence in Limnology, Exercise Physiology, Sports Journalism, Creative Arts Education, French Language Education, Emergency Medicine na Dental Prosthodontics.

Kwa ujumla, majukumu ya Tutorial Assistant ni kuwasaidia na kujifunza kutoka kwa wahadhiri wakuu kupitia mihadhara, semina, mafunzo na vitendo, kushiriki katika tafiti, ushauri wa kitaalamu na huduma kwa jamii, pamoja na kuendelea na mafunzo ya uzamili kwa ajili ya shahada ya uzamili.

Waombaji wanatakiwa kuwa na shahada ya kwanza inayohusiana na nafasi wanayoomba na kuwa na wastani wa ufaulu wa GPA usiopungua 3.8 kutoka chuo kinachotambuliwa na Tanzania Commission for Universities (TCU).

Baadhi ya nafasi zina viwango vya mshahara vya PUTS 1.1, PUTS 1.2 na PUTS 1.3, huku ajira zikitolewa kwa masharti ya kudumu na yenye mafao ya pensheni.

Masharti ya waombaji

UDSM imesema waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45. Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na wanapaswa kujitambulisha wazi kupitia mfumo wa maombi.

Waombaji wanatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA), pamoja na kuwasilisha wasifu binafsi (CV), nakala zilizothibitishwa za vyeti na transcript za masomo, cheti cha kuzaliwa na majina pamoja na anwani za wadhamini wawili.

Aidha, waombaji wenye vyeti kutoka vyuo vya nje wanatakiwa kuhakikisha vyeti hivyo vimethibitishwa na TCU, huku vyeti vya elimu ya sekondari kutoka nje vikithibitishwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Chuo kimeonya kuwa utoaji wa vyeti vya kughushi au taarifa za uongo utasababisha mwombaji kuondolewa kwenye mchakato wa ajira na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Jinsi ya kutuma maombi

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia Recruitment Portal ya Serikali kwa kutumia  na si kwa njia nyingine.

Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuelekezwa kwa Deputy Vice Chancellor (Academic), University of Dar es Salaam, P.O. Box 35091, Dar es Salaam.

Mwisho wa kutuma maombi ni Agosti 18, 2026.

UDSM imesema waombaji wote, waliochaguliwa na ambao hawakuchaguliwa, watajulishwa kupitia akaunti zao katika Ajira Portal.

Leave a Comment