×

Yanga Yatwaa Ngao ya Jamii 2026 Baada ya Kuichapa Simba 1-0

ZANZIBAR: Young Africans SC (Yanga) wameanza msimu mpya kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, na kutwaa Ngao ya Jamii 2026 katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Ushindi huo umeifanya Yanga kutwaa taji hilo kwa mara ya 10 katika historia ya michuano ya Ngao ya Jamii, huku wakifikisha idadi sawa na Simba SC ambao pia wamelibeba taji hilo mara 10.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 31 na Albert Kangwanda, ambaye aliwapa Wananchi uongozi ambao uliodumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo.

Simba walijaribu kurejea mchezoni na kutafuta bao la kusawazisha, lakini Yanga waliendelea kuwa imara katika safu zao na kuhakikisha wanaulinda ushindi huo hadi filimbi ya mwisho.

Kwa Yanga, ushindi huu unaongeza morali ya kikosi hicho kinachoanza msimu wa 2026/27 kikiwa na lengo la kuendeleza ubabe wao katika soka la Tanzania.

Kwa upande mwingine, Simba SC watalazimika kusubiri nafasi nyingine baada ya kushindwa kulipa kisasi dhidi ya Yanga, ambao msimu uliopita pia waliwafunga kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Matokeo ya Mchezo

Yanga SC 1-0 Simba SC

31′ Albert Kangwanda

🏆 Yanga SC – Mabingwa wa Ngao ya Jamii 2026

Taji hili limekuwa la 10 kwa Yanga katika historia ya Ngao ya Jamii, hivyo kuifanya rekodi yao kufikia idadi sawa na Simba SC.

Leave a Comment