
Adhimisho hilo limefanyika katika Viwanja vya Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na waumini kutoka maeneo tofauti.Misa hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, ambaye alikuwa Askofu kiongozi katika uwekaji wakfu huo.Amehudumu pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya, pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu.

Sherehe hiyo ya kidini pia imewakutanisha Maaskofu kutoka majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki nchini, viongozi wa madhehebu tofauti ya Kikristo, viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali.
Aidha, Mapadre, Watawa, familia, ndugu, marafiki na waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini wamehudhuria kushuhudia tukio hilo muhimu katika Kanisa Katoliki.

Kuwekwa wakfu kwa Mhashamu Vincent Mpwaji kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam ni hatua muhimu katika huduma yake ya kiroho na uongozi wa Kanisa, huku akitarajiwa kushirikiana na viongozi wengine katika kutekeleza majukumu ya kichungaji ndani ya Jimbo hilo.




