×

Viongozi Mbalimbali Wamfariji Rais Samia Kizimkazi – Picha

KIZIMKAZI, ZANZIBAR: Viongozi mbalimbali wa dini, taasisi za umma na binafsi pamoja na makundi mbalimbali wameendelea kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Viongozi hao wamefika nyumbani kwa Rais Samia Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 11 na 12, 2026, kwa ajili ya kutoa pole na kumfariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Miongoni mwa waliofika ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi, ambaye alifika Kizimkazi kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake.

Aidha, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ni miongoni mwa viongozi wa dini waliomtembelea Rais Samia na kumpa pole kufuatia msiba huo.

Viongozi mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi pia wamefika nyumbani hapo kuungana na Rais Samia pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo.

Mbali na viongozi hao, mabondia kutoka Mafia Boxing nao wamefika Kizimkazi kutoa pole na faraja kwa Rais Samia kufuatia msiba wa mume wake.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ziara hizo za viongozi na makundi mbalimbali zinaendelea kuonyesha mshikamano na kutoa faraja kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi. 

Leave a Comment