×

Mpiga Picha Mkongwe na Mwanzilishi wa ITV, Mzee Abdalah Haji Afariki Dunia

 

MPIGA picha mkongwe na mmoja wa waajiriwa waanzilishi wa ITV, Mzee Abdalah Haji, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Bi. Asha Abdalah Haji, Mzee Abdalah Haji amefariki dunia leo saa 11 jioni katika Hospitali ya Global, Unguja, ambako alikuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi, figo na shinikizo la damu.

Mzee Haji alijiunga na ITV mwaka 1994 akitokea  ambako alikuwa akifanya kazi kama mpiga picha mwandamizi.

Katika kipindi cha utumishi wake TVZ, Mzee Haji alishiriki katika kurekodi matukio mbalimbali muhimu, ikiwemo matukio ya Vita vya Uganda vilivyotokea mwaka 1978.

Mwaka 1994, alikuwa miongoni mwa waajiriwa waanzilishi wa ITV, akishiriki katika safari ya mwanzo ya kituo hicho cha televisheni na kuendelea kufanya kazi hadi alipostaafu.

Mwili wa marehemu Mzee Abdalah Haji unatarajiwa kupumzishwa kesho huko Unguja, Zanzibar.

Marehemu ameacha watoto tisa na mjukuu mmoja.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Leave a Comment